Tuesday, January 27, 2015

enjoy kiduchu

pumzikeni kwa amani watoto

mama mmoja mkazi wa tabora amewauwa watoto wake wawili kwa madai kuwa mwanaume amemkimbia na yeye ameamua kuwauwa hao watoto ili abaki peke yake hana uwezo wa kuwahudumia watoto,
watoto hao mwamvua mrisho miaka 4 na mdogo wake sudi miezi 4 walikutwa wamefukiwa ndani ya nyumba waliokuwa wakiishi
 
 loooh sijui dunia inaelekea wapi jamani kweli kabisaaa mi hata siekewi. unaanzaje kuwauwa wanao uliowazaa kwa uchungu kwa kisingizio kuwa hutoweza kuwahudumia
na nyie wanaume aliyesema wanawake ndio wakulea watoto peke yao ni nani? kama huwezi kuwahudumia hebu waachane wabaki na Mungu kwani huko wanapatiwa kila hitaji sio kuwaleta duniani na kuwatesa jamani
eeeeeeeeeeeeeeMungu tuhurumie sie waja wako
hatujajua tuyatendao yanakukera kwa kiasi gani
 pumzikeni kwa amani watoto