Wednesday, May 28, 2014

R.I.P Rachel Raule

poleni wana bongo movie na watanzania wenzangu kwa ujumla. ila pole zaidi kwa familia ya Rachel. jamani kama mwanamke ambaye nafatilia kwa karibu uhusianao wa mama na mtoto as my blog say hii imeniuma saana.
     kupoteza watu wawili kwa wakati mmoja ni uchungu mkubwa ambao binadamu anatakiwa kuukabili maana tunaamini ni mapenzi ya mungu pia
         lakini ni mpaka lini tutakuwa tunalia na vifo vya mama na mtoto au mama au mtoto? tufike wakati watanzania wanawake tusiine kubeba mimba ni nusu ya kifo jamani wanawake wengi tumewapoteza katika uzazi
        hebu tufikie hatua ya mtu kutamani kubeba mimba na kuwa na uhakika wa kujifungua salama na kurudi kwake salama/ saaawa tunajua kuna Mungu ambaye anaamua lini amchukue nani katika style ipi but sometime tunaweza kujitahidi katika mengine haswaaa katika maswala ya mama na mtoto
             pleeeease serikali yetu tunaomba mjitahidi kwa hili ingawa mnasema mmepunguza vifo vya uzazi kwa aslilimia kazaa tunaomba ifike asilimia 00.
       kwa kumbukumbu yangu huyu ni msanii wa pili wa kike anayekufa kwa swala la uzazi mwingine ni yule muimbaji wa taarabu.
 swwwwwwwwwwwwwwwaaali je hao ambao hawajulikani ni wangapi kwa siku wanafariki?
             chonde chonde mtulinde wanawake na watoto jamani ni nguzo ya taifa lolote dunian
               bila mwanamke hakuna mtoto bila mtoto hakuna kijana bila kijana hakuna taifa.
 TANZANIA BILA VIFO VYA UZAZI INAWEZEKANA   
           ANZA   SASA KUTIMIZA WAJIBU WAKO
 MKUNGA TIMIZA WAJIBU WAKO
 MAMA TIMIZA WAJIBU WAKO
 SERIKALI TIMIZA WAJIBU

No comments:

Post a Comment