GAIDI MTANZANIA SHAMBULIZI LA GARISA NI
MWENYEJI WA MWANGA
Taarifa zinazoendelea kutolewa na vyombo vya
usalama vya Kenya zimesema Rashid Charles
Mberesero aliyekamatwa kuhusika na shambulizi
la kigaidi lililofanywa na wapiganaji wa kikundi
cha Al-Shabab kwenye chuo kikuu cha Garisaa
ambapo watu 148 wameripotiwa kuuawa,
anatokea Usangi katika wilaya ya Mwanga mkoa
wa Kilimanjaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya amesema
kwamba Rashid alikamatwa akiwa amejificha juu
ya dari la moja ya majengo ya chuo cha Garissa
ambapo baada ya uchunguzi ilidhihika kuwa
hakuwa mwanafunzi wala mkaazi katika chuo
hicho. Pia alipokamatwa alipatikana akiwa na
mabomu kadhaa ya milipuko.
Kufuatia taarifa hizi Mbunge wa Mwanga ambaye
pia ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe alisema “Nimeshtushwa sana na
taarifa hizi. Ninaufahamu ukoo wa Mberesero
ambao wanafamila wake wengi ni wakristo. Kwa
wakati huu ni vyema tukaviachia vyombo vya
usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu
suala hili.”
Rashidi
Charles ni mjukuu wa mzee Mberesero mmiliki
wa kampuni ya Ngorika bus,kwao ni Kisangara
Mwanga na siyo Usangi.kinacho shangaza siyo
dini bali utulivu aliokuwa nao huyo kijana,huwezi
kudhania ni kwanini amejiingiza kwenye vitendo
hivyo kwavile kama ni swala la pesa kwao
zimejaa.ama kweli umdhanie siye ndie.
sasa, huyo rashid mberesero ni mtoto wa Charles mberesero wa mke wa nje na nasikia anasema walifunga chuo Dodoma wakaenda Kenya kwa ajili ya kuvamia chuo cha garissa, huko Kenya walikutana na wenzao (wasomali) na walikuwa tarehe tano wavamie uwanja wa taifa dsm kulikuwa na tamasha la pasaka.
Wednesday, April 8, 2015
UGAIDI GARISA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment